title : Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe
kiungo : Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe
Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe
Na. MWANDISHI WETU – DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.
“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.
Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.
“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi Dodoma.
Afisa Mtendaji Kata Bw. John Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko Kigwe kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Bahi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe lililofadhiliwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na Halmashauri wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama Wilayani Bahi Dodoma.
Hivyo makala Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe
yaani makala yote Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/waziri-mhagama-aitaka-halmashauri-ya.html
0 Response to "Waziri Mhagama aitaka Halmashauri ya Bahi kukamilisha ujenzi wa Soko la Kigwe"
Post a Comment