CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461
kiungo : CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

soma pia


CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461


Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi ya Mbeya Desemba 8 na Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam Desemba 22. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mahafali hayo, Dk. Mrisho Malipula na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Mrisho Malipula, akitoa ufafanuzi juu ya mahafali hayo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akitoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Baraza la Masajili 'Convocation' utakaofanyika Novemba 29, 2017 Kampasi Kuu Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.


Morogoro, Tanzania-Novemba 27


MAHAFALI ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30, 2017, jumla ya wahitimu 3,461 katika mwaka wa masomo 2016/2017 wanatarajiwa kutunukiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas samatta, kati ya wahitimu hao ni

*Shahada ya Uzamivu (PhD) ni 4 (0.12%)

*Shahada za Umahiri (Masters) ni 1,005 (29.04%)

*Shahada za Kwanza (Bachelors) ni 2,063 (59.61%)

*Stashahada (Diploma) ni 191 (5.52%)

*Astashahada (Certificate) ni 198 (5.72%).


Kati ya wahitimu wote waliohitimu Kampasi Kuu ni 2,119 (61.23%).

Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Mbeya ni 734 (21.21) na Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Dae es Salaam ni 608 (17.57%).

Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika Kampasi Kuu Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi Mbeya Desemba 8 2017 na Chuo cha Kampasi Dar es Salaam Desemba 22 2017.

Mahafali hayo yatatanguliwa na mkutano wa 17 wa baraza la Masajili Çonvocation' utakaofanyika Novemba 29 2017 katika ukumbi wa mihadhara wa Fanon, uliopo kampasi Kuu. Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwaka 2002 na wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.

Mjadala mahususi na nafasi ya wahitimu na wanachuo katika kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe utafanyika.

Aidha Baraza la Masajili linaendelea kuwahamasisha wahitimu wote wa Chuo Kikuu Mzumbe na wadau wengine kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa kike kupitia 'Çonvocation Fundraising Account'namba 01o150209448900 iliyopo Benki ya CRDB, Tawi la Mzumbe.


Hivyo makala CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

yaani makala yote CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/chuo-kikuu-mzumbe-kutunuku-shahada.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461"

Post a Comment