title : mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar
kiungo : mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar
mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema utamaduni wa watu wa Zanzibar wa kuheshimu dini zote ni nguzo imara iliyosimamisha amani na utulivu nchini.
Balozi Seif ameyasema hayo afisini kwake Vuga wakati akipokea msaada wa fedha taslim shilingi milioni 10 kwa ajili ya sekta ya afya kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini.
Amesema tangu zamani waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu wamekuwa wakiishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii bila ya mikwaruzano.
Amesema msaada huo wa fedha ambao umekusudiwa kwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja umekuja wakati muwafaka ambapo Serikali imo katika mipango ya kuimarisha huduma zote zitolewazo hospitalini hapo.
Akikabidhi msaada huo wa shilingi milioni 10 kwa Makamo wa Pili wa Rais, mchungaji Bariki Urassa amesema madhehebu yao ya Efatha hupeleka misaada yake pale inapohitajika.
Amesema wakati wa ziara ya kiongozi wao Mkuu wa Efatha Duniani mchungaji Josephate Elias Mwingira alipoonana na makamo wa Pili wa Rais aliahidi kuisaidia Hospitali ya Mnazi Mmoja, ahadi ambayo amekuja kuitekeleza kwa niaba yake.
Sherehe fupi ya makabidhiano ya msaada huo ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah ambaye kwa niaba ya Wizara yake ameahidi kuutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa.
Katibu Mkuu huyo amesema Wizara yake itatoa mashirikiano ya karibu kwa wale wote wanaotaka kuchangia na kutoa wito kwa taasisi nyengine za ndani na nje kujitokeza kutoa misaada yao kwa Wizara yake ambayo imepewa majukumu makubwa ya kuwahudumia kifya wananchi wote wa Zanzibar.
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akipokea msaada wa fedha taslim shillingi milioni 10 kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha kwa ajili ya hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akionesha msaada huo wa fedha taslimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah
Hivyo makala mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar
yaani makala yote mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mchungaji-bariki-urassa-wa-madhehebu-ya.html
0 Response to "mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar"
Post a Comment