title : BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’
kiungo : BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’
BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’
Abiria wanaotumia usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam sasa hawatosumbuka tena kuhusu kutembea na fedha taslim mfukoni au usumbufu wa makondakta wa kutokua na chenchi, lakini pia wamiliki wa daladala wataanza kuona faida katika uwekezaji wao, kutoana na kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kukusanya nauli kielektroniki uliozinduliwa na Kampuni ya BCX chini ya bidhaa yake ya ‘Uhuru Pay’.
Tanzania inakuwa nchi ya nne Afrika kuzindua huduma hii baada ya Malawi, Zambia na Msumbiji ambako tayari imekwisha anza kutumika.
Mfumo huu wa ulipaji wa nauli kielektroniki una lengo la kurahisisha usafiri kwa watumiaji wa usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam kwa kuwapa fursa ya kulipia nauli kwa kutumia kadi. Kama mradi wa majaribio mfumo huu utaanzishwa kwanza kwenye ruti ya Tegeta Nyuki na Kivukoni kabla ya kuhamia kwenye maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BCX-Tanzania, Seronga Wangwe alisema ‘Uhuru Pay’ inalenga kurahisisha ulipaji wa nauli kwa wasafiri wa daladala na kuhakikisha kuwa abiria wanasafiri kwa utulivu na amani.
Tofauti na hilo ni kuwa wamiliki wa daladala wataweza kupata faida katika uwekezaji wanaofanya kwenye mabasi hayo kutokana na udhibiti na uwazi wa mapato yanayokusanywa”.
Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Ebenezer Massawe (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipa nauli kielektroniki kupitia huduma mpya iliyozinduliwa na Kampuni hiyo ya 'Uhuru Pay' wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika leo jijiji Dar es salaam. Toka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BCX Tanzania, Seronga Wangwe, Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi.
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Business Connexion (BCX) Tanzania, Seronga Wangwe (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Christiania inayomiliki daladala zinazofanya safari zake kati ya Tegeta Nyuki na Kivukoni hapa jijini Dar es salaam, Emmanuel Mlaponi kwa kukubali kutumia huduma mpya ya ‘Uhuru Pay’ kwa ajili ya malipo ya nauli kielektroniki wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia toka kushoto ni Afisa wa BCX, Justin Lawena, Meneja Masoko na Mauzo wa Business Connexion (BCX), Ebenezer Massawe na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geoffrey Silanda
Mkurugenzi Mtendaji wa Business Connexion (BCX) Tanzania , Seronga Wange akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja Mauzo na Masoko wa BCX, Ebenezer Massawe na kulia ni Afisa wa Kampuni hiyo, Justin Lawena.
Hivyo makala BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’
yaani makala yote BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/bcx-yazindua-uhuru-pay.html
0 Response to "BCX YAZINDUA ‘UHURU PAY’"
Post a Comment