WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA
kiungo : WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

soma pia


WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.


Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.

Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

“Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”

Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.

Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.




Hivyo makala WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA

yaani makala yote WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/watanzania-watakiwa-kujiepusha-na-dawa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA DAWA ZA KULEVYA"

Post a Comment