title : AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI
kiungo : AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI
AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI
Wazazi hususani jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu, badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu, jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu kutokana na kufichwa huko
“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususani walemavu, wanawanyima haki yao, mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi, hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina
mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo (habari picha na woindeshizza blog )
Mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo.
Hivyo makala AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI
yaani makala yote AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/amina-mollel-wazazi-msiwafiche-watoto_6.html
0 Response to "AMINA MOLLEL: WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI"
Post a Comment