title : WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA.
kiungo : WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA.
WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani vikali mauaji ya watoto wawili ambao walitekwa na kukutwa wameuawa katika mkoa wa Arusha.
Wizara imepokea taarifa ya vifo hivyo kwa simanzi kubwa na inalaani vikali mauaji hayo ambayo yamekatisha uhai wa watoto hao katika umri huo mdogo. Mauaji na utekaji waliofanyiwa watoto hawa ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Mtoto ikiwemo haki ya Kuishi ambayo ndiyo haki kuu kati ya haki zote.
Wizara inawaasa wazazi, walezi na jamii kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto katika ngazi ya mitaa, vijiji na jamii ili kuwa na mifumo madhubuti katika kudhibiti ukatili unaofanywa dhidi ya watoto na kusababisha majonzi makubwa kwa wazazi, familia na jamii kwa ujumla.
Jamii inakumbushwa kuwa tatizo la utekaji wa watoto linahitaji juhudi za pamoja katika kupambana nalo ili kuzifanya jamii zetu kuwa mahala salama kwa watoto wetu kuishi. Wizara itaendelea kuimarisha Kamati za ulinzi na usalama wa Mtoto katika ngazi za kata, vijiji na mitaa ili kuboresha huduma za ulinzi wa watoto wetu.
Aidha, Wizara inalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zilizofanyika za kutaka kuwaokoa watoto hao wakiwa hai, ingawa juhudi hizo hazikufanikiwa.
Wizara inaomba wazazi, walezi, familia, walimu na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/09/2017.
Hivyo makala WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA.
yaani makala yote WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/wizara-ya-afya-yalaani-mauaji-ya-watoto.html
0 Response to "WIZARA YA AFYA YALAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI WALIOTEKWA MKOANI ARUSHA."
Post a Comment