title : Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu
kiungo : Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu
Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu
Na: Frank Shija – MAELEZO
Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimeanzisha huduma ya Dawati la Mhasibu itayaofanyika kwa mara ya kwanza tarehe 07 Oktoba 2017 kuanzia saa 3: 00 asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaaam.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Msemwa amesema kuwa kupitia Dawati hilo wahasibu, wataalam wa kodi, fedha na biashara watajumuika pamoja na kukutana na wananchi wa kawaida, wafanyabiashara wadogo na wakubwa na kuwapatia huduma bure.
“Kupitia Dawati hili la Mhasibu litatukutanisha na wadau wengine wa masuala ya biashara na ujasiriamali hili kwa pamoja tuweze kutoa huduma za mbalimbali za kijasiriamali zianazohusisha masuala ya mahesabu bila ya malipo” alisema Dkt. Msemwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dkt. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Dyoya James Dyoya na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dyoya James Dyoya (kushoto) akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu na Mweneyekiti wa chama hicho Dkt. Fred Msemwa.
Hivyo makala Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu
yaani makala yote Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wakazi-dar-kunufaika-na-huduma-ya.html
0 Response to "Wakazi Dar Kunufaika na Huduma ya Dawati la Mhasibu"
Post a Comment