title : Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda
kiungo : Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda
Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda
Na Thobias Robert- MAELEZO
Bodi mpya ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kusimamia vyema majukumu yake ya upatikanaji wa rasimali watu wenye weledi, sifa na haiba ambao wataisaidia serikali katika kufikia azma yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angelah Kairuki alipokuwa akizindua bodi hiyo Jijini Dar es Salaam na kuitaka kuendesha kazi zake kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu.
“Mmeteuliwa katika kipindi cha miaka michache kabla ya Taifa letu kufikia mwaka 2025 ambapo tunalenga kuingia kwenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo mnalo jukumu kubwa la kulipatia taifa rasilimali watu yenye uwezo wa kutuwezesha kutimiza malengo hayo,” alifafanua Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki alisema kuwa, katika kutekeleza majukumu yake bodi haina budi kutenda haki ili kuepuka malalamiko ya upendeleo wa aina yoyote, kujuana, ukabila, na ukanda ambavyo vimekuwa vikitolewa dhidi ya bodi ya Sekrtarieti ya Ajira,na kuwataka kuandaa mpango mkakati ambao ukitumika kila mwombaji wa ajira ataridhika.
Katibu wa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma Bw. Xavier Daudi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki jinsi ya ufanyaji kazi wa menejimenti hiyo katika uzinduzi wa Bodi mpya uliofanyika leo katika Maktaba Kuu ya Taifa Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro akitoa salama na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kutoa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro.
Mwenyekti wa Bodi mpya ya Sekritarieti ya Ajira katika utumishi wa umma Bi.Rose Lugembe katika uzinduzi wa tatu wa bodi pamoja na mkataba wa huduma kwa mteja uliofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni moja ya wajumbe wa bodi hiyo Bw.Mbaraka Abdul Wakill.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO.
Hivyo makala Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda
yaani makala yote Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/bodi-ya-sekretarieti-ya-ajira-yatakiwa.html
0 Response to "Bodi ya Sekretarieti ya Ajira Yatakiwa kuisaidia Serikali Katika Ajenda ya Viwanda"
Post a Comment