title : WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB
kiungo : WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB
WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB
Wafanyabiashara wadogo na wakati wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiinua kiuchumi kwa kuchukua mkopo inayotolewa na benki ya CRDB ndani ya siku saba.
Akizungumza kwenye sherehe za ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja duniani, meneja wa CRDB tawi la Babati Ronald Paul alisema mkopo huo wa miezi mitatu utawanyanyua kiuchumi wajasiriamali hao. Paul alisema wajasiriamali hao wachangakie fursa hiyo ambayo imeanzishwa wiki hii ya huduma kwa wateja dunia, ambapo pia itaendelea kutolewa na benki hiyo kwa siku zote zinazoendelea kuwepo.
Alisema wamejipanga kuboresha zaidi huduma kwa wateja wa benki yao, hivyo wajasiriamali wa mjini Babati, wilaya za Kiteto, Mbulu, Simanjiro, Hanang' na miji midogo ya Mirerani, Magugu, Galapo, Haydom na Dareda, wachangakie fursa hiyo.
Alisema wiki ya huduma kwa wateja dunia, itafikia kileleni jumamosi ijayo mjini Babati, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera ambaye atazungumza na wadau wa benki ya CRDB."Siku hiyo kutakuwa na shamrashamra za kutosha kwani wadau wenye ushawishi kwa jamii watakuwepo kwenye tawi hili la CRDB Babati, ambapo watatueleza mambo mawili matatu yatakayowanufaisha wajasiriamali wetu," alisema Paul.
Aliwaahidi wateja wa benki hiyo kuwa huduma zimeboreshwa zaidi hivyo wafike na kujionea wenyewe kwa kuweka fedha, kufungua akaunti au kuchukua mikopo, kwani hata riba zao ni nafuu tofauti na taasisi nyingine za fedha. Mmoja kati ya wajasiriamali wa mji mdogo wa Magugu wilayani Babati, Elizabeth Seluhinga alisema huu ndiyo wakati wa kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Seluhinga alisema yeye ni mjasiriamali wa nyanya kwenye mji mdogo wa Magugu na anatarajia kuchukua mkopo kwenye benki ya CRDB ambapo ameambiwa ndani ya siku saba atakuwa ameshapatiwa fedha za mkopo.
Alisema wajasiriamali wasiogope kuchukua mikopo ili kuboresha biashara zao kwani hata wafanyabiashara maarufu nchini, wengi wao wamenyanyuka kimaisha kwa kuchukua mikopo na siyo vinginevyo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye viwanja vya benki yao tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wao kwenye wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi ijayo.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Ronald Paul, akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi Ijayo.
Hivyo makala WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB
yaani makala yote WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wajasiriamali-manyara-watakiwa.html
0 Response to "WAJASIRIAMALI MANYARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO CRDB"
Post a Comment