TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.

TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.
kiungo : TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.

soma pia


TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.

Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

JIJI la Dar es Salaama ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi kubwa duniani, huku ukuaji huo ukiathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo sekta ya usafirishaji.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 inakadiria kuwa jiji la Dar es Salaam lina wakazi milioni 2.4 na kuwa na kiwango cha ongezeko la idadi ya watu cha asilimia 4.4 kwa mwaka huku ongezeko hilo likisababisha kujitokeza kwa mapungufu katika utoaji wa huduma mbalimbali.

Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo kuanzisha barabara za njia moja, kuanzisha maegesho ya magari ya kulipia, na kuhamasisha kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.

Pamoja na jitihada za serikali ya jiji la Dar es Salaam na serikali kuu kuboresha usafiri Jijini humo, bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati wa saa za asubuhi na jioni ambapo ambapo ilimlazimu mwananchi kuchukua takribani masaa matatu, kwa mfano, kutoka Mbezi Juu hadi katikati ya jiji.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam imekuwa ikitekeleza miradi maalum ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu za Jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Miradi wa Ofisi ya TANROAD Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius Ngusa anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam wa awamu ya tatu ni moja ya mikakati ya Serikali ya kushughulikia tatizo sugu la msongamano wa magari katika Jiji hilo ambapo utekelezaji wake ulianza tangu wa mwaka wa fedha 2008/2009.

Anasema kupitia mradi huo, Serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya kujengwa katika kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Ubungo Bus Terminal-Kigogo-Kawawa (6.4 km), barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner (km 12), barabara ya Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi mwisho (10 km), Tanki bovu-Goba (9.0 km), Kimara baruti-Msewe-Changanyikeni (2.6 km).

Anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi/Morogoro (km 20) , Kigogo Round about-Jangwani-Twiga katika bonde la msimbazi (km 2.72), Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External (Mandela) (2.25 km).

Mhandisi Ngusa anasema miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika tangu mwaka 2008.
Anaitaja miradi iliyokamilika ni pamoja na barabara ya Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 11.44, barabara ya Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 7.64 ambayo ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis Corner iliyokamilika mwaka 2011.

“Kuhusu Awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, ujenzi wake ulianza mwaka 2014 ambapo hadi sasa kazi za ujenzi zilizokamilika kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi Bovu (Samaki Wabichi)-Goba km 9 ilikamilika mwaka 2016 kugharimu kiasi Tsh. Bilioni 8.6 ” anasema Ngusa.



Hivyo makala TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM.

yaani makala yote TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/tanroad-imekuja-na-suluhu-ya-tatizo-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANROAD IMEKUJA NA SULUHU YA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJI LA DAR ES SALAAM."

Post a Comment