title : Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa
kiungo : Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa
Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa
Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania, kuwa ndio nchi inayoongoza nchi zote za Afrika ya Mashariki, kwa matumizi ya mifumo ya malipo kwa njia ya Mtandao, kulipia huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara na wakati huo, kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano wa kuingwa na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki, katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, ambaye amesema kupitia ufadhili wa TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, na kile cha Zanzibar, (ZNCCIA) kumeifanya Tanzania kuwa ndio nchi ya kwanza kunufaika na kufaidika na mfumo madhubuti na wa kisasa wa usajili vyeti vya uhalisia (certificate of orgin) na kuripoti vikwazo vya kibiashara kwa kutumia simu za mkononi, wakati wa halfa ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo, kwa njia ya Mtandao kwa TCCAI ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, uliofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanya biashara zaidi ya 200.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, "Sisi kama TMEA tuna furaha kubwa kusaidia mfumo huu wa LIPA FASTA kufanya kazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania, hivyo kukuza biashara na kuleta ufanisi wa biashara kwa Tanzania. Ulanga amesema TMEA imetumia zaidi ya Dola za Marekani, $ 600,000 katika kufanikisha mradi huu kwa kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, lakini pia unahusisha Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Zanzibar, (ZNCCIA), F
fedha za kugharimia mpango huu, zimetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la kimataifa, (DFID) kupitia TradeMark, East Africa, (TMEA) inayosimamia utekelezaji wa mradi huo. Ulanga amesema maboresha ya biashara, yanafungua zaidi fursa za Watanzania kufanya biashara, kilichobaki ni kwa Watanzania kuchangamkia fursa hizo, kwa hoja kuwa fursa hazingoji mtu, tukishindwa kuzichangamkia fursa hizi, zitachangamkiwa na wengine.
Kwa upande wake, Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja amesema "Tunaishukuru sana TMEA kwa misaada wa kugharimia mfumo huu, muhimu ambao utaokoa muda na kupunguza gharama, kwani muda ni mali muhimu sana kwa mfanyabiashara yoyote, ukiokoa muda, umeokoa fedha na umeongeza faida”, hivyo LIPA FASTA itaongeza kasi ya usajili wa vyetu vya uasili kuongeza kasi ya kufanya biashara.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuzindua Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi Kulipia huduma za TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga (wa pili kulia) na Makamo rais wa TCCAI, Joseph Kahungwa (kulia)
Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga (katikati) akiteta jambo na Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa (TMEA), kulia ni Makamo rais wa TCCAI, Joseph Kahungwa (kulia).
Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa
Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki uzinduzi wa Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi kulipia huduma za vyeti vya uhalisia, vinavyotolewa na TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi Raymond Mbilinyi, (katikati) kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara, baada ya kuzindua Mfumo wa malipo kwa mtandao, kutumia simu za mkononi Kulipia huduma za TCCIA ujulikanao kwa jina la LIPA FASTA, katika hafla ya uzinduzi mfumo huo iliyofanyika jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mfumo huo umefadhili wa na TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA.
Hivyo makala Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa
yaani makala yote Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/taasisi-ya-trademark-east-africa.html
0 Response to "Taasisi ya Trademark East Africa, imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania yapongezwa"
Post a Comment