title : serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega
kiungo : serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega
serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema serikali ya Viwanda inakwenda na ufugaji Kuku pamoja na samaki kwa kutengeneza Viwanda vya Kuku pamoja na mabwawa ya ufugaji samaki.
Ulega aliyasema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwenye vijiji vinne, ambapo alisema hakuna sababu ya wananchi wa Mkuranga kuchukua Kuku mikoa mingine wakati wanaweza kufuga wenyewe na kujipatia kipato na maendeleo yakapatikana na kuwawezesha kuuza hata sehemu nyingine.
Amesema yuko tayari kuwasaidia wananchi wa Mkuranga mbegu za Kuku pamoja na watalaam wa kuwafundisha jinsi ya kufanya ufugaji wa Kuku na samaki wa kisasa. Amesema ajira katika Wilaya hiyo zipo ikiwa ni pamoja na ufugaji Kuku pamoja na samaki ambayo ni ajira ya kudumu na soko ni kubwa kutokana mahitaji ya vitoweo hivyo kuhitajika kwa wingi.
"Sioni sababu wananchi wa Mkuranga kuchukua kuku kutoka mikoa mingine wakati mnaweza kufanya nyinyi wenyewe kutokana na maeneo mlionayo, haitawezekana kama nyinyi hamtaweza kuonyesha mfano nikiwa ni Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi"alisema Ulega.
Katika ziara yake alitembelea Ujenzi wa Zahanati za Kibamba, Kimazichana na Mwandege na kuahidi kuwaunga mkono wananchi katika juhudi mbalimbali wanazoonyesha katika maendeleo ya huduma za jamii. Ulega amesema kuwa wakati uliopo ni kufanya kazi za Maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya dhamira ya serikali ya Viwanda.
Naibu waziri aliaahidi kuchagiaji sh. Milioni moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha VICCOBA cha wanawake waliojenga ukumbi wa mikutano na sherehe kilichopo Mwandege.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibamba juu ya maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kimazichana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiangalia ufugaji wa Kuku katika eneo la Rabica ,Kibamba.
Hivyo makala serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega
yaani makala yote serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/serikali-ya-viwanda-viwanda-ni-pamoja.html
0 Response to "serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega"
Post a Comment