title : Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha
kiungo : Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha
Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha
Serikali yawataka watanzania kurejesha nchi katika misingi iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuwa na viongozi waadilifu,wazalendo na wenye uchungu na nchi yao.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 18 ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ole Nasha amesema kuwa kumekuwa na ombwe kubwa la kuporomoka kwa maadili, kushamiri kwa rushwa, ufisadi, kukosekana kwa uzalendo na uwajibikaji, kuwepo kwa wafanyakazi hewa na biashara ya madawa ya kulevya.
Ameongeza kuwa wengi waliokuwa wakiharibu nchi hii ni watanzania wenyewe kwa ajili ya tamaa na ubinafsi wao. Nimefarijika sana kusikia kuwa Chuo kimeanza kurejesha hadhi yake iliyokuwepo hapo awali kilipoasisiwa kwa kuanzisha program maalum ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora,”alisema Ole Nasha.
Akizungumzia Mada Kuu ya Kongamano ambayo ni Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri amesema kuwa ni ukweli usiopingika katika uchumi wa maendeleo ya viwanda, Uzalendo, Utaifa, Uadilifu na Uongozi Bora vinapaswa kuzingatiwa. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa viwanda si maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha
yaani makala yote Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/rejesheni-uadilifu-uzalendo-nchini-ole.html
0 Response to "Rejesheni Uadilifu, Uzalendo Nchini- Ole Nasha"
Post a Comment