Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa.

Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa.
kiungo : Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa.

soma pia


Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za filamu za Watanzania nchini unakomeshwa mara moja kwa kuwasaka wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema ambapo moja ya changamoto kubwa aliyotajiwa na wamiliki hao ni suala la uharamia wa kazi za sanaa jambo ambalo linawakwamisha wamiliki hao kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakivujisha filamu mpya kwa kuziuza kiholela mitaani na wengine wakihuisha filamu hizo katika mitandao ya kijamii jambo linalosabibisha hasara kubwa kwa wasanii na wamiliki wa majumba ya sinema.

Mhe. Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu hao wanaojihusisha na uharamia wa kazi za filamu za Watanzania huku akiapa kuwashughulikia popote walipo watu hao ili kuhakikisha kuwa Wasanii wananufaika na kazi zao na pia Wamiliki wa Majengo ya Sinema wananufaika pia kwa kuonyesha kazi za wasanii hao kwa utaratibu ambao hautomuumiza msanii mwenye kazi yake.

“Najua baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Sinema mnapata hasara, na hata baadhi ya Wasanii pia, suala hili linanikera sana na kamwe haikubaliki hata kidogo, tutahakikisha kwamba watu wa namna hii wanatoweka katika tasnia yetu, tutawasaka popote walipo na kuwapeleka kwenye vyombo vya Sheria kwani Serikali hii sio ye mchezo na watu wa namna hii”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa, yeye kama Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo atahakikisha kwamba hamasa ya kutosha inatolewa kwa Watanzania ili wawe na utamaduni wa kuangalia sinema zinazotengenezwa nchini katika Majumba ya Sinema yaliyopo nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa katika moja ya Jumba la Kuonyeshea Sinema lililopo Jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo, Bibi Leah Kihimbi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (kushoto) wakiangalia moja ya kifaa kikubwa kitumikacho kuonyeshea sinema maarufu kama Projekta wakati walipokutana na Wamiliki wa Majumba hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa wameongozana na baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM).



Hivyo makala Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa.

yaani makala yote Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/dkt-harrison-mwakyembe-aahidi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Dkt. Harrison Mwakyembe aahidi kuwatokomeza Waharamia wa Kazi za Filamu kwa maslahi ya Wasanii na Taifa."

Post a Comment