title : WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG
kiungo : WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG
WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.
Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG, Bw…….. amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao umeanza Novemba 29, 2017 na kubeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo Bw. Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha leo Novemba 30, 2017.
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza
Mkurugenzi wa Fedha WA WCF, Bw.Bezil Kwala, akiwasilisha ripoti ya fedha ya Mfuko kwa mwaka wa 2015-2016.
Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ofisi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Johanes Joel Kisiri, akisikiliza uwasilishaji wa taarifa hiyo ya fedha.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria juu ya kuanzishwa kwa Mfuko na jinsi unavyofanya kazi zake. Pamoja na mambo mengine Bw. Siyovelwa aliwaambia wajumbe kuwa, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoazishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura Na. 263 (Marejeo ya 2015) na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015. Lengo la kuazishwa kwa Mfuko ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta rasmi (Binafsi na Umma) Tanzania bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG
yaani makala yote WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/wcf-yapata-hati-safi-katika-ukaguzi-wa.html
0 Response to "WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG"
Post a Comment