title : MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA
kiungo : MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA
MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.
Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.
“Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati
Kabati alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu binafsi” alisema kabati
Aidha Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule hizo.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kuzitambua changamoto za shule za msingi.
Hivyo makala MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA
yaani makala yote MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mbunge-ritta-kabati-kukarabati-shule-za.html
0 Response to "MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA"
Post a Comment