MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA

MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA
kiungo : MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA

soma pia


MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA

Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mh. Abdalah Hamisi Ulega ameitaka Halmashauri ya wilaya Mkuranga kushirikiana na wananchi kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji.

Akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika ziara yake ya wilayani Mkuranga mkoani Pwani alisema tatizo la wakulima na wafugaji ni changamoto kubwa kwahiyo ni muhimu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili wasizagae hovyo.

Ametaka maafisa mifugo wasikae maofisini bali waende kutoa huduma vijijini na kuwasiliza wananchi kero zao.Ulega amesema vikundi vya wafugaji wakina mama na vijana vipewe kipaumbele, vitambuliwe na kudhaminiwa kwenye utoaji mikopo kwa ajili ya kuinua kipato na kuongeza pato la taifa na la mtu mmoja mmoja

"Tunahitajika tutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji, na hii ni changamoto tunayotakiwa kuifanyia kazi hatupaswi kuwaacha wafugaji wakihamahama" amesema Ulega. 

Aidha alisema kuwa Halmashauri inatakiwa kufanya utafiti na kupima ardhi ambayo watawatengenezea miundombinu bora kwa ajili ya wafugaji. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga, Filiberto Sanga alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ardhi, wananchi wanauza ardhi kiholela kiasi kwamba wanakosa maeneo ya kilimo hivyo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo. 

Sanga alisema kuwa agizo la naibu waziri wamelipokea japokuwa wanauhaba wa ardhi lakini wameanisha baadhi ya maeneo yaliyopo tarafa ya Mkamba ambayo watayafanyia utafiti kwa ajili ya wafugaji. 
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuhusu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, filiberto Sanga akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kuwa na maeneo ya kilimo. 
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi alipokutana nao na kufanya mazungumzo kuhusu usawa na wajibu wa kila mtu ili kufikia malengo ya taifa kiujumla mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho leo mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).


Hivyo makala MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA

yaani makala yote MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/maafisa-mifugo-msikae-ofisini-nendeni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAAFISA MIFUGO MSIKAE OFISINI NENDENI KUTOA HUDUMA VIJIJINI: NAIBU WAZIRI ULEGA"

Post a Comment