title : Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI
kiungo : Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI
Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella lipo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).
Hayo yameelezwa leo Octoba 30 na wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuja kwa ajili ya kutajwa,
"Mheshimiwa, jalada halisi la kesi hii limetoka ofisi ya upelelezi mkoa wa Temeke (RCO) na sasa lipo kwa DCI." Amesema Mwita.
Kufuatia Maelezo hayo,, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, mwaka huu pia ameusisitiza upande wa Mashtaka wakamilishe mapema upelelezi.
Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka huu, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Tukio hilo, linalodaiwa kufanyika Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao, awali Februari 23, 2016, waliachiwa huru katika kesi ya mauaji namba 32 ya mwaka 2016 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa.
Baada ya kufutwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikifanana na hii walikamatwa na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.
Hivyo makala Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI
yaani makala yote Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/jalada-kesi-ya-mke-wa-marehemu-bilionea.html
0 Response to "Jalada kesi ya mke wa marehemu bilionea msuya liko kwa DCI"
Post a Comment