title : PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO
kiungo : PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO
PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ( kulia) akipatiwa maelezo ya maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018, usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani kutoka kwa Meneja mradi wa Kampuni ya Yapi Merkezi , Kemal Artuz.
Na John Nditi, Kibaha
WAZIRI wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini Uturuki inayojenga reli ya kisasa (Standard Gauge)’SGR’ kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro urefu wa kilomita 300 kuongeza kasi na kufanya kazi mchana na usiku ili ujenzi huo ukamikike kwa wakati kulingana na makubaliano ya kimkataba.
Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushitukiza Juni 5, mwaka huu ( 2018) majira ya saa tano siku kwenye kambi ya Reli ya Mwendokasi iliyopo Soga , wilayani Kibaha mkoani Pwani na kuendesha ukaguzi hadi saa sita usiku maeneo mbalimbali ya ujenzi wa njia ya SGR.
Alisema , lengo la kufanya ziara ya kushitukiza ni kujionea namna walivyojipata kuhakikisha kazi zinafanyika saa 24 mchana na usiku ndani ya siku saba za juma.
Profesa Mbarawa alisema , lengo ni kuona makubaliano kati ya mkandarasi na Serikali ya kukamilishwa kwa ujenzi huo ifikapo Novemba mwaka 2019 unatimizwa na wananchi kunufaika na mradi huo mkubwa.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akijandaa kuelezea maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018 usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani .
Hata hivyo , Waziri aliwakuta wafanyakazi na wahandisi wa mradi huo wa kiwa maeneo yao ya kazi , ambapo aliwataka watanzania walipata fursa ya kusimamia kazi hiyo kuwepo eneo la mradi kipindi chote cha saa 24 na kupangiana zamu za kazi .
Alisema , hatua hiyo itawezesha shughuli ya ujenzi iendelee kwa kasi zaidi na kwa muda wote kama ilivyopangwa ndani yamakubaliano na kazi hiyo inafanyika kwa viwango vya ubora na ufanisi mkubwa.
Pamoja na hayo alitumia fursa hiyo kumkata mkandarasi wa ujenzi huo kupitia Meneja mradi , Kemal Artuz kuogeza kasi ya ujenzi ili kufikiwa makubaliano ya kukamilishwa kwa ujenzi wa reli hiyo kwa wakati kuwezesha watanzania kunufaika na matunda hayo.
Kwa mujibu wa Waziri ,njia ya reli ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro urefu wa kilometa 300 na kati ya hizo, kilometa 205 ni eneo la njia ya reli na nyingine 95 ni za kupishana na mradi huo utagharimu kiasi cha Sh trrioni 2. 7.9.
“ Tayari wameanza kujenga tuta na sehemu nyingine wameweka kokoto kabla ya kuweka mataaluma , kazi inaenda vizuri “ alisema Profesa Mbarawa na kuongeza .
“ Tuta linalojengwa linapaswa liwe na vipimo na viwango vilivyokubalika kwa pamoja kimkataba ili reli hii ya kisasa inayotumia umeme itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria ” alisema Profesa Mbarawa.
Waziri alisema , treni ya mizigo itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa kilometa 120 kwa saa na kubeba mizigo tani 10,000 kwa wakati mmoja na kwa maana hiyo itaweza kuondoa barabarani mizigo tani 20 kwa magari 500 wakati mmoja. Profesa Mbarawa alitaja kipande cha reli kingine kitakachojengwa ni kutoka Morogoro- Makutupola chenye urefu kilometa 422 .
Waziri Mbarawa alisema ,reli ya kwendo kasi itakayokuwa imejengwa kutoka Dar es Salaam hadi Makutupola itakuwa na urefu wa kilometa 722 na ujenzi wake utagharimu kiasi cha Sh trrioni 7.06.7 fedha zinagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.
Naye Mhandisi na Msimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa , Josephat Rutaihwa alisema, kazi za ujenzi huo inaenda kwa kasi kutokana na vifaa kuwepo eneo la mradi hadi kufikia Juni 5, 2018 kazi zilizofanyiwa ni asilimia 13 ya ujenzi wa mradi mzima wa kilometa 205 kutoka Dar es Salaam hadi Ngerengere.Hata hivyo alimhakikishia Waziri kuwa , kazi hiyo inakwenda kama ilivyoangwa na kwamba mradi huo utakamilishwa ndani ya mkataba Novemba 2, 2019.
“ Kazi niafanyika mchana na usiku kama mlivyotukuta na mheshimiwa Waziri … na inafanyika kwa ubora na umakini na sasa tumefikia kwa baadhi ya maeneo kumwaga kokoto na baada kuweka mataaluma “ alisema Mhandisi Rutaihwa.
Hivyo makala PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO
yaani makala yote PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/prof-mbarawa-afanya-ziara-ya-kushtukiza.html
0 Response to "PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO"
Post a Comment