title : ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU
kiungo : ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU
ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU
Mwambawahabari
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akiongea na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wa pili kushoto mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam , wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa ESA Bi. Catherine Sozi na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi mwakilishi nchini Leo Zekeng
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na baadhi ya wadau wa afya kutoka Shirika linaloshughulikia maswala ya ukimwi kutoka Umoja Wa Mataifa(UN Aids) na Wizara ya Afya , kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe
Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wa kwanza kulia akiongea na baadhi ya watendaji wa sekta ya Afya hawapo pichani wakati alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam , kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe mara baada ya maongezi wakati alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wa pili kulia , wengine ni Mkurugenzi mwakilishi nchini Leo Zekeng wa kwanza kushoto na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kanda ya ESA Bi. Catherine Sozi mara baada ya maongezi wakati alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Ubora wa Hudum za Afya nchini Dkt. Mohammed Mohammed kushoto akifuatilia mazungumzo kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa maongezi na Mkurugenzi Mtendaji wa UN Aids Bw. Michael Sidibe hayupo pichani , kulia ni Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt. Neema Rusibamayila .
………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Asilimia 95 ya kina mama wajawazito hufikiwa na huduma ya kupima maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) ili kuweza kujifungua salama watoto ambao hawana hatari ya kupata maambukizi hayo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wakati alipotembelea ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam leo.
“Hata hivyo asilimia 90 ya walio na maambukizi wamepata dawa za ARV hii imepelekea maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto kupungua katika asilimia 21 mwaka 2009 hadi 7.6 mwaka 2015” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisisitiza kuwa tunaweka nguvu zaidi kwa vijana na hasa wa kike na vijana walio katika makundi maalum yenye hatari zaidi ya kuambukiza au kuambukizwa VVU.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika mapambano zidi ya UKIMWI ili kufikia malengo ya kutokomeza janga hilo la kiafya katika jamii ifikapo mwaka 2030 kwani maambukizi yamepungua toka asilimia 7.1 mwaka 2007/8 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/12.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe amesema kuwa wafadhili wanachangia sehemu kubwa ya muitikio wa mapambano ya UKIMWI hivyo UNAIDS wako tayari kusaidia katika kuandaa mpango endelevu ili kuhakikisha Fedha za wafadhili zikipungua huduma ziendelee.
Aidha Bw. Sidibe amesema kuwa Shirika la UNAIDS limeanzisha mpango wa kuwezesha nchi za Afrika kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya Jamii ambao watasaidia kuboresha mfumo mzima wa Sekta ya Afya.
Mbali na hayo Bw. Sidibe ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika mapambano ya UKIMWI nchini, hususani kuweza kufikia takribani Waathirika 935,228 wanaotumia dawa za ARV ifikapo Juni 2017.
Hivyo makala ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU
yaani makala yote ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/asilimia-95-ya-kina-mama-wajawazito.html
0 Response to "ASILIMIA 95 YA KINA MAMA WAJAWAZITO HUFIKIWA NA HUDUMA YA KUPIMA VVU"
Post a Comment