title : DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA
kiungo : DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA
DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA
Na Ripota Wetu,Nyasa
SEPTEMBA 8 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kutafanyika tamasha kubwa la harambee ya kuchangia elimu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi hasa wakike kwa ajili ya Wilaya ya Nyasa.
Tamasha hilo ambalo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo lengo likiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi huo wa mabweni.Akizungumza leo wilayani nyasa Mkuu wa wilaya hiyo Esabela Chilumba amesema anawakumbusha wadau wote wa elimu kuendelea kuchangia.
Amesema siku zinazidi kusogea hivyo wote waliopewa bahasha maalum za kuchangia anawakumbusha kuendelea kuchangia kwa njia mbalimbali ambazo zimewekwa wazi kwa ajili ya kukusanya fedha hizo." Binafsi niwaombe wadau mbalimbali waendelee kutoa michango yao lengo nikufanikisha harambee hiii ambayo lengo hasa nikukusanya Sh. bilioni moja ambazo zitatumika kujenga mabweni hayo,"amesema Esabela
Ameongeza kupitia kamati na akaunti mbalimbali zilizowekwa wazi wadau waendelee kuchangia kwani watoto wakike wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mimba za utoto." Ndugu mwandishi kama nilivyosema awali kutokana na watoto wengi kuishi mazingira ya mbali na shule inapelekea waliowengi kukatisha masomo kwasababu ya kupata mimba za utoto,"amesema
Amesema mbali na mimba wengine wanashindwa kumaliza shule kwa sababu ya utoro unaotokana na kuishi mbali naazingira ya shule hivyo nivema wakajitokeza kwa wingi kuchangia.Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa wilaya ambayo ipo pembezoni mwa Ziwa Nyasa ambapo shughuli zake kubwa ni uvuvi na kilimo hivyo kujengwa kwa mabweni kutasaidia wanafunzi wa kike kukaa shule na mwisho wa siku kufanya vizuri katika masomo yao.
Pia Chilumba amewataka wananchi wa wilaya hiyo ya Nyasa kuendelea kushikamana na kudumisha usalama ukizingatia ni wilaya ambauyo ipo mpakani na pia waendelea kuchapa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao huku wakiunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.
Hivyo makala DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA
yaani makala yote DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/dc-nyasa-awakumbusha-waliopewa-bahasha.html
0 Response to "DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA"
Post a Comment