title : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI
kiungo : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI mkuu,Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na ngazi nyingine mkoani Pwani,kujikita kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na watanzania kijumla.
Amesema haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu wasiojulikana wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu ,na ni hatari endapo watajiingiza katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma yao.
Aidha Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji kutathmini matokeo ya mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na kama sheria inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha asimilia 50 ya utekelezaji.
Waziri huyo ,pia ameziagiza halmashauri nchini kuona umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya kununua magari ya zimamoto yatakayosaidia kudhibiti majanga ya moto yanapotokea hususan kwenye maeneo ya uzalishaji na viwanda.
Katika hatua nyingine amelitaka shirika la umeme Tanesco,Dawasco kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya umeme na maji katika maeneo yenye uwekezaji ili kuvutia wawekezaji.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,wakati alipowasili katika kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS kilichopo Pichandege Kibaha Mjini.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa viwanda vya kutengeneza sabuni cha KEDS Pichandege Kibaha Mjini ambae pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze,Jack Feng.Picha na Mwamvua Mwinyi
Hivyo makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI
yaani makala yote WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ulinzi.html
0 Response to "WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA-ULINZI UIMARISHWE KWENYE MAENEO YA VIWANDA NA UWEKEZAJI"
Post a Comment