title : UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU
kiungo : UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU
UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya tafiti ya asali zilizokusanywa zenye chembechembe za nikotini kuwa zimefanyiwa majaribio na zimedhihirisha kuwa chembechembe hizo ni chache sana na hazina uwezo wa kudhuru mwili wa binadamu.
Akizungumza na Vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Glory Mziray amesema TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila baada ya miaka miwili kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye Maabara za kimataifa na mara zote zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko yote ya kitaifa na kimataifa.
Amezitaja tafiti mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa lengo lake lilikuwa ni kuainisha madhara ya ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na ameyataja maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa ni mkoa wa Tabora na Kigoma
Mziray amesema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango cha nikotini kinachopatikana kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali ilivyochavushwa na mimea mingine kama vile nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha nikotini hakina madhara kwa binadamu.
Amesema watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini kwenye asali kwa kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini asali za Tanzania zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini.
Mziray amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile asali ni chakula cha kiasili kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea mbalimbali.Ameongeza kuwa, asali ni mchanganyiko uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na vitamin.
Baadhi ya Sampuli ya asali inayopatikana katika maeneo mbalimbali za nchi. Asali hutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu.
Hivyo makala UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU
yaani makala yote UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/utafiti-kiwango-cha-nikotini.html
0 Response to "UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU"
Post a Comment