title : Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kiungo : Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Na Maura Mwingira , Ihumwa Dodoma
Mama Regina (55) ni kati ya akina mama takribani kumi, ambao ni sehemu ya vibarua wanaoshiriki kwa kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za kubeba zege katika eneo la Ihumwa inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Eneo hili la Ihumwa na ambalo lipo takribani kilometa 17 kutoka Dodoma Mjini, limetengwa maalum kuwa Mji wa Kiserikali ambapo kunajengwa Majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.
“Karibu habari za kazi” ananisalimia mama huyu ambaye anajitabulisha kama Mama Regina wakati nilipomsogelea mahali alipokuwa akichota maji kutoka kwenye simutanki kubwa lililopo eneo la Ujenzi.“ Unataka kunipiga picha” ananiuliza Mama Regina, baada ya kuniona nimeshika Kamera. Ni kamjibu kama yuko tayari na ananiruhusu kumpiga picha”.
Ninapomuuliza kuhusu kazi yake, Mama Regina kwa tabasamu kubwa ananijibu “ Ninamshukuru Mungu, nimefika leo asubuhi na nikabahatika kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi huu, ninashukuru sana tunafanya hivi kwa ajili ya ada za watoto” anasema Mama Regina kwa furaha kubwa.Furaha ya Mama Regina ya kupata nafasi ya kushiriki kazi ya ujenzi inajithihirisha wazi wazi usoni mwake ni furaha pia inayonekana kwa wamamawegine wanaobeba zege
Anajitishwa ndoo yake ya maji kichwani na kuniambia . “ Mimi nakaa kijiji kingine mbali kidogo na eneo hili la ujenzi, kwa hiyo ilinipasa kufika mapema asubuhi na nikapata nafasi, Kwa kweli nina mshukuru Mungu”
Mwandishi wa habari hii alikuwa miongoni mwa Maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokwenda jana ( Alhamisi) kuangalia na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.
Akina Mama wakiwa bega kwa bega na vibarua wenzao wanaume katika kubeba zege linalotumia kwa ujenzi wa msingi na nguzo za jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma

Kazi ya uchanganyaji zege ikiendelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ihumwa.( Picha na Habari kwa Hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)

Mama Regina akijitwika ndoo ya maji na kuipeleka kunakoojengwa Msingi. Mama Rejina anasema anamshukuru Mungu kwa kupata fursa ya kushiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama ilivyo kwa akina mama wengi, Anasema kazi hiyo anaifanya kwaajili ya watoto wake ( ada)

Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiangalia na kukagua maendeleo ya ujenzi wa msingi na usimikaji wa nguzo mwenye kofia nyekundu ni Injinia Shadrack Ng’wiza kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Corporation Sole ( Works Superntent) kutoka Mwanza.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Hivyo makala Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
yaani makala yote Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wanawake-wanavyoshiriki-ujenzi-wa-ofisi.html
0 Response to "Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali"
Post a Comment