Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu

Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu
kiungo : Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu

soma pia


Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu


Spika Ndugai leo amewausia wabunge wanzake kuwa makini na usalama wao kwa kuchukua hatua zaidi za kujilinda, ikiwemo kutokaa baa mpaka usiku wa manane ili kujiepusha na matatizo mbali mbali yatakayoathiri usalama wao. .

Akizungumza muda mfupi leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai aliwataka wabunge kutokaa sana katika mabaa.

“Yaani tuchukue hatua tu katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe kwanza,”amesema.

Amesema vyombo vya usalama vinavyowalinda vinakuwa vinaongezea kidogo na kuwataka kutazama nyendo zao za namna ambavyo wanaishi.

“Kwa wale tuliozoea sana saa 7 ndio tunarudi nyumbani  basi tuanze kurudi mapema kidogo. Lakini pia tuangalie usalama wa familia zetu na tuwaambie wapigakura naona siku hizi watoto wanapotea, watoto wanauawa,”amesema.

Amewataka wabunge kuwapelekea huo ujumbe kuwa wawe makini na watoto wao wakati wa kwenda shule na maeneo mengine kwa kuhakikisha wanajua mtu anayewapeleka shule na kuwachukua.

“Hayo mambo yanayofanana na hayo. Ushauri ni wa ujumla tu,”amesema.

Aliwataka wabunge kuendelea kumuombea Tundu Lissu na wale watakaopata nafasi ya kwenda kumuona jijini Nairobi wampelekee ujumbe.

Amesema pia wabunge wawaombee wenzao ambao wamekwenda kumuuguza mbunge huyo lakini wanatukana kwa sababu hawajui watendalo.

Ushauri huo umekuja siku chache baada ya Lissu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.


Hivyo makala Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu

yaani makala yote Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/spika-ndugai-awatahadharisha-wabunge.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Spika Ndugai Awatahadharisha wabunge kuhusu Usalama Wao na Kutokaa Baa Muda Mrefu"

Post a Comment