SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM

SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM
kiungo : SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM

soma pia


SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na kusema kuwa yoyote atakaye jihusisha na vitendo vya Rushwa asitegemee nafasi ndani ya jumuiya hiyo au chama
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari juu ya mwenendo wa Jumuiya hiyo nchini na mafanikio waliyoyapata ndani ya miaka mitatu
 Waandishi wa  Habari walioshiriki mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shakha Hamdu Shakha.


Ndugu Waandishi wa habari;

Kwa mara nyingine tena tunawakaribisha kwa mikono miwili katika mkutano huu muhimu. Karibuni sana huku nikiwaomba  mjione mko huru na mko nyumbani .

Dhana ya Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama na  Jumuiya zake. Kiongozi wa UVCCM mahali popote pale huchaguliwa kwa kufanyika uchaguzi huru na wa  haki unaozingatia Kanuni na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoagizwa na vikao husika bila ya kukiuka, kupuuzwa au kuvunjwa.

Nia ya UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba  njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya kweli , yenye kuchunga  adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

April Mwaka 2017 Chama Cha Mapinduzi kilianza mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama na Jumuiya zake. Kufuatia mabadiliko ya Kanuni ya UVCCM yaliyofanyika mwezi Machi, 2017 tulianza Uchaguzi katika ngazi za Matawi ambapo hadi leo jumla ya Matawi 23,529  sawa na Asilimia 99.4% kati ya Matawi  23,670 sawa na Asilimia 0.59% yamekamilisha uchaguzi.
Ngazi za   Kata  3,913 sawa na Asilimia 96.59% kati ya Kata 4,051 sawa na asilimia 3.4% zimekamilisha uchaguzi .Kwa upande wa majimbo ya  Zanzibar majimbo 54 sawa na Asilimia 100%, wamekamilisha uchaguzi.  

Ngazi ya Wilaya na Mkoa  mchakato wa uchujaji wa  majina kwa Vijana waliomba nafasi mbali mbali ndani ya Jumuiya yetu , umeanza na  unaendelea vizuri huku jumla ya Vijana 7,606 wamejitokeza kuchuka fomu za kugombea nafasi mbali mbali katka Jumuiya yetu, hali inayoonyesha kumekupo kwa mabadiliko  na msisimko wa kisiasa ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

Kwa upande wa ngazi ya Taifa Vijana 350 wamejitokeza kuomba nafasi za uongozi ndani ya UVCCM kama ifuatavyo:-

(i) Nafasi ya Mwenyekiti 113 Walioomba
(ii) Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa 24 Walioomba
(iii) Nafasi 5 za Wajumbe wa H/Kuu 103 Walioomba
(iv) Nafasi  5 za Wajumbe wa B/Kuu Taifa 81 Walioomba
(v) Nafasi 1 Wawakilishi UWT 14 Walioomba
(vi) Nafasi 1 Wawakilishi Wazazi 15 Walioomba


Hivyo makala SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM

yaani makala yote SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/shaka-awaonya-watakaojihusisha-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SHAKA AWAONYA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA KWENYE CHAGUZI ZA UVCCM"

Post a Comment