title : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
kiungo : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
Alisema kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa nchi wananchama wa Afrika Mashariki lina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na kubadilishana utalaamu .
Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
Samia alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu. “Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili “Alisema Makamo wa Rais.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/makamu-wa-rais-samia-suluhu-hassan_6.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment