MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA

MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA
kiungo : MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA

soma pia


MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA

Na Tiganya Vincent

KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Tabora imezuia vifaa vya ujenzi vya Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege na kunyang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili hadi watakapomalizia malipo ya waliokuwa wafanyakazi wao.

Uamuzi huo umetolewa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipokuwa akitoa maamuzi ya  wajumbe wake kwenye mkutano na viongozi wa Kampuni hiyo na wanaodai.

Alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Mhasibu wa Kampuni hiyo Bw. Mahmut Garik kukataa kutoa vielelezo vinavyoonyesha  jinsi alivyowalipa waliokuwa wafanyakazi wao ili kuona kama madai ya wafanyakazi hao ni halali au sio halali.
Mwanri alisema kuwa zoezi la kushughulikia madai ya wafanyakazi hao ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea Uwanja wa Ndege mkoani Tabora kuonyeshwa bango la kumdai mmiliki wa Kampuni na ndipo Rais aliagiza lishughulikiwe.

Alisema kuwa wakati wa majadiliano baina ya pande zote tatu yakiendelea na ndipo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipomwomba Mhasibu wa Kampuni hiyo kuwasilisha vielelezo vinavyoonyesha ushahidi wake kama kweli alisha walipa wafanyakazi wake na ndipo alipojibu kuwa hawezi kutoa labda waendee Mahakamani.

“Kitendo hicho cha kuonyesha jeuri hakiwezi kukubalika…RPC hakikisha hatoi vifaa vyake na Uhamiaji chukua Hati zao za kusafiri …hadi ukweli ujulikane…maana wakishaondoka Tabora ..wananchi hawa hawawezi kuwapata” alisema Mwanri
Kwa upande Meneja Mradi wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun  Ercan Kavaic aliomba radhi kwa kauli ya Mhasibu wake ya kukataa kutoa nyaraka hizo ambazo ndio zingesaidia kuondoa mvutano huo.

Aliahidi kukaa pamoja na wadai wake na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa ili kupitia madai na kuna njia bora ya kutatua tatizo hilo. Kavaic alikubali vifaa vyake kuwa chini ya ulinzi na kutoa hati yake ya kusafiria hadi hapo watakapopata muafaka.

Kwa upande wa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze aliwashauri vijana wanaomba kazi katika Kampuni mbalimbali za ujenzi wakahakikisha wanapewa mikataba kabla mradi haujaanza ili wajue malipo na stahili wanazopaswa kupata ili  kuondoa migogoro wa malipo pindi wanapokuwa wamemaliza mkataba.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa hakuna kifaa kitakachoondoa katika eneo la mradi hadi hapo wakapokuwa wamehakikishiwa kuwa mgogoro ulipo wa malipo umemalizika.


Hivyo makala MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA

yaani makala yote MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/madai-ya-wafanyakazi-yasababisha-vifaa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MADAI YA WAFANYAKAZI YASABABISHA VIFAA VYA UJENZI VYA KAMPUNI YA CEYTUN KUZUIWA UWANJA WA NDEGE TABORA"

Post a Comment