title : Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini.
kiungo : Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini.
Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini.
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kocha mkuu wa timu ya Soka ya Kombain ya Mjini Unguja Mohammed Seif “King” amejiuzulu kuifundisha timu hiyo baada ya kupata mafanikio makubwa kwa miaka 3 mfululizo tangu alipoanza kuifundisha kikosi hicho .
Sababu kubwa iliyomfanya akae pembeni kocha huyo ni mafanikio makubwa aliyoyapata na kusema kwasasa anawapa nafasi makocha wengine kuifundisha timu hiyo.
“Nawapa nafasi makocha wenzangu kuifundiasha timu hii, nimeongoza kwa mafanikio makubwa, kwasasa nimeamua kukaa pembeni kwani hapa Wilaya ya Mjini kuna makocha wengi bora na wenye sifa ya kuifundisha timu hii, sasa ni fursa na wao kwao kwani mimi nimeongoza kwa mafanikio makubwa”. Alisema King.
Kocha King alianzaa kuifundisha timu hiyo tangu mwaka 2015 ambapo alitwaa kombe la Wilaya za Zanzibar, mwaka 2016 akatwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza kwenye Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone ambapo Mjini Unguja walishinda kombe hilo kule Arusha na mwaka huu 2017 akashinda tena kombe hilo huko wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
Kwasasa Kocha huyo anafundisha timu ya Miembeni City ambayo inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja.
Hivyo makala Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini.
yaani makala yote Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/kocha-king-ajiuzulu-kuifundisha.html
0 Response to "Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini."
Post a Comment