title : BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018
kiungo : BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018
BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018
BODI ya Korosho Tanzania imetangaza bei elekezi kwa msimu 2017/2018 kwa kilo moja ya Korosho ghafi daraja la kwanza (Standard Grade) kitakuwa ni sh.1,450 huku kilo moja ya daraja la pili itakuwa ikiuzwa kiasi cha sh.1,160.
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa soko la Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.
"Niseme tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.
Alisema kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni 1,208.39 na asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .
Aidha alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018 ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni 143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni tsh.1,593.50.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah katikati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga leo kuhusu bei elekezi ya korosho msimu wa 2017/2018 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Maokola Majogo 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)Hassani Jarufu
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia
Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku Yusuph wa Gazet la Tanzania Daima,Amina Kingazi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub wa Mwananchi.
Hivyo makala BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018
yaani makala yote BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/bodi-ya-korosho-tanzania-yatangaza-bei.html
0 Response to "BODI YA KOROSHO TANZANIA YATANGAZA BEI ELEKEZI KWA MSIMU WA 2017/2018"
Post a Comment