title : WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA
kiungo : WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA
WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA
Na Agness Moshi na Bushiri Matenda –MAELEZO.
Watanzania na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini wameombwa kuendelea kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora.
Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Tulia Trust Mhe.Tulia Akson, wakati akikabidhi msaada runinga nne na katoni mbili za maziwa vyenye thamani ya shilingi 1,000,000 vilivyotolewa kwa watoto waliopo kwenye Taasisi hiyo kwa ushirikiano na Dstv, TSN na Kampuni ya Twincity.
Dkt.Tulia amesema msaada wa runinga unatimiza ahadi waliohaidi kwa taasisi hiyo na unamaana kubwa sana kwa sababu utawasaidia watoto wanaokaa hospitalini hapo kwa muda mrefu kujifunza ,na kuwaburudisha kwa kipindi chote cha matibabu ya awali kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Watoto hawa wanakaa muda mrefu hospitalini wakitibiwa hivyo wanashindwa kujumuika na wenzao kwa michezo jambo ambalo linawafanya wahisi upweke kwa kuwapatia runinga kutawasaidia kuondoa hali hiyo , kuwaburudisha na kuwapa nafasi ya kujifunza kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na king’amuzi cha DSTV”, alisema Dkt.Tulia
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt.Mohammed Janabi amesema kuwa si watoto tu watakaofaidika kwani hata wazazi wao wataweza kujua mambo mbalimbali yanayoendelea Nchini kwa kuangalia taarifa za Habari zitakazokua zinaonyeshwa kupitia chaneli mbalimbali.
“ Sio watoto wote wanaokuja hapa wanatatizo la moyo peke yake wengine wanakuja wakiwa na Magonjwa mengine ambapo inabidi tuanze kuwatibia kwanza magonjwa hayo ambapo wakati mwingine yanachukua muda mrefu hivyo basi kwa kipindi chote hicho runinga hizi zitakua zikiwapa burudani, elimu kwa masomo mbalimbali kama vile kiingereza, hesabu kwa watoto wakubwa na kwa wale wadogo wataburudika kupitia katuni”,alisema Dkt.Janabi.
Dkt.Janabi ameongeza kuwa msaada wa maziwa waliopewa utasaidia kuimarisha afya za watoto wadogo wanaotibiwa kwani wapo wengine wamekuja wakiwa na Afya duni ,wengine wana magonjwa ya utapia mlo hivyo kupelekea kuchelewa kupatiwa matibabu.
Aidha,Dkt.Janabi amemshukuru Dkt.Tulia kupitia Mfuko wake wa Tulia Trust kwa kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuipatia misaada Taasisi hiyo.
Kwa upande wake mtoto Mwamvita Hassani mwenye umri wa miaka 13 kutoka wilayani Kondoa kwa niaba ya watoto wanaotibiwa kwenye Taasisi hiyo ametoa shukrani zake kwa Naibu Spika na wadau waliowapa misaada hiyo.“Ninawashukuru sana kwakutuletea Tv na Maziwa,Tumefurahi na tunawaombea watuletee Tv zingine”, alisema Mwamvita.
Dkt.Janabi amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia upatikanaji wa vitanda kwa ajili ya Taasisi hiyo kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo swala la upungufu wa vitanda kwa wagonjwa kwani wanavitanda 128 tu ambavyo havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu.
Hivyo makala WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA
yaani makala yote WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/watanzania-tuendelee-kuichangia-taasisi.html
0 Response to "WATANZANIA TUENDELEE KUICHANGIA TAASISI YA JKCI: DKT.TULIA"
Post a Comment