title : WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR.
kiungo : WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR.
WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR.
WADAU wa maji na Mazingira washauriwa kushirikiana ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pia washauriwa kutoa namba maalumu ya simu kwaajili ya wananchi waonapo tatizo la maji au maji kutiririka katika maeneo mbalimbali ili kuondoa upotevu wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akizungumza na wadau wa maji pamoja na wadau wa Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Wadau wamaji wanatakiwa kushirikiana na ili kupunguza upotevu wa maji kutokana na ubovu wa miundo mbinu ya maji.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, usambazaji wa maji
Haruni Josef Kwa upande wake DAWASCO wamewaomba wadau wa maji ili kuendeleza na kukuza maendeleo ya kwaajili ya kujenga mtandao wa maji kwaajili ya kuyasafirisha ili yamfikie kila mwananchi wa jiji la Dar es Salaam.
Wadau waliokutana leo ni Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wizara ya Afya, DAWASCO,DAWASA, WATERAID na wadau wa mazingira kwa pamoja wakiwa na kauli mbiu ya maji ni uhai na usafi ni utu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wadau wa maji safi pamoja na wadau wa maji taka ili kutatua changamoto za maji katika jiji la Dar es Salaam.Pia ameshuhudia kusaini makubaliano kati Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Taasisi ya Borda ya hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akishuhudia taasisi ya Borda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya wadau ya maji wa maji safi na wazingira walipokutana leo leo kufanya mazungumzo ya wadau wa maji pamoja na wadau wa mazingira.
Wawakilishi wa Kampuni ya Jamka Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi milioni Tano ambazo wamekopeshwa na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) leo mara baada ya kikao cha Wadau wa Maji na Mazingira kufunguliwa jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzungumza masuala ya maji na mazingira.
Hivyo makala WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR.
yaani makala yote WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/wadau-wa-maji-washauriwa-kushirikiana.html
0 Response to "WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR."
Post a Comment