title : BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI
kiungo : BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI
BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, leo tarehe 10/6/2018 amepokea ugeni wa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.
Mapema akimkaribisha mgeni wake, DC Mgandilwa amemshukuru Balozi Najem kwa moyo wake wa upendo kwa watanzania hususani wakazi wa Kigamboni.
Ameeleza kuwa vifaa ambavyo vimetolewa ni vya zaidi ya Shilingi milioni kumi na moja na vinalenga kuondoa changamoto iliyokuwepo katika wodi za akina mama na watoto.
Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na mashine za kusaidia wakati wa upasuaji, mashine za kusaidia kupumua, vifaa vya kupima moyo, vitanda vya watoto na beseni maalum kwa ajili ya akina mama wanaojifungua.
DC Mgandilwa amesema kuwa nchi ya Kuwait ni miongoni mwa nchi ambazo ni marafiki wazuri wa Tanzania na kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni itaendeleza ushirikiano huo mwema.
Kwa upande wake, Balozi Jasem Al Najem amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kigamboni kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakimpatia mara zote alipotembelea wilaya hiyo.
Balozi Jasem ameeleza kuwa vifaa tiba alivyovikabidhi sio msaada bali ni zawadi kutoka kwa watu wa Kuwait kwenda kwa marafiki zao walioko Tanzania.
Balozi Najem ameongeza kuwa huo ni mwanzo tu kwani baadhi ya vifaa tiba vingine vilivyoombwa na DC Mgandilwa atahakikisha vinapatikana na kuletwa ili kusaidia watu wa Kigamboni na watanzania kwa ujumla.
Hafla ya kukabidhi vifaa tiba imefanyika katika hospitali ya Vijibweni na baadae DC Mgandilwa alimkaribisha mgeni wake iftar iliyoandaliwa katika viwanja vya Msikiti wa Gaddafi uliopo Kigambobi.
Hivyo makala BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI
yaani makala yote BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/balozi-wa-kuwait-akabidhi-vifaa-tiba.html
0 Response to "BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI"
Post a Comment