title : TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI
kiungo : TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI
TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza kitu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa majisafi na majitaka jijini Dar es salaam
Kaimu Mkurugenzi WaterAid Henry Horombe akihojiwa na wanahabari katika mkutano huo
|
Kufuatia changamoto za huduma bora za Majisafi na Majitaka katika jiji la Dar es salaam Serikali imeamua kukutana na wadau mbalimbali ili kuweza kujadili namna ya kuzikabili changamoto hizo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema aliyezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ambapo amesema kuwa ili kuendana na malengo ya Serikali ya kuhakikisha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanapata huduma ya maji ifikapo mwaka 2020 ni lazima kukaa na wadau mbalimbali kujadili na kufikia maazimio ambayo yatakuwa suluhu ya matatizo ya maji jijini humo.
Amesema maji yanayozalishwa hivi sasa ni mengi na yanakidhi zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji hivyo basi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuweza kupata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2020 iwapo watakaa na wadau wote kuona namna bora ya ufanisi wa kuyasambaza maji yote yanayozalishwa hivi sasa.
"Leo tumekutana na baadhi tu ya wadau wetu wa Maendeleo ambao wamekuwa wanatusaidia sana katika suala zima la kuhakikisha tatizo la maji linapungua",alisema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa maji DAWASCO Mhandisi Aron Joseph amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikia asilimia 95 ya usambazaji wa maji jijini humo ifikapo mwaka 2020 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa WaterAid Henry Horombe ambao ndio wadhamini wa mkutano huo amesema zaidi ya shilingi Bilioni 17 zinahitajika katika mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza changamoto mbalimbali za majisafi.
"Tunajitahidi kuja na njia tofauti za kuweza kuwafanya wadau waweze kukutana na kujadili pamoja na kuweza kufikia malengo kwa muda mfupi zaidi",alisema.
Aidha DC Mjema amewashukuru WaterAid kwa kuweza kufadhili kikao hicho ambapo amesema anatambua kuwa wadau wote walioshiriki wanatambua kuwa wananchi wa Dar es salaam wana kiu ya huduma bora ya maji.
|
Hivyo makala TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI
yaani makala yote TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/tatizo-la-maji-safi-na-maji-taka-dar.html
0 Response to "TATIZO LA MAJI SAFI NA MAJI TAKA DAR LATAFUTIWA UFUMBUZI"
Post a Comment