SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI

SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI
kiungo : SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI

soma pia


SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Kanuni za taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Crossborder Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ambapo wasafirishaji wa fedha taslimu na wasafiri wote wanaotoka au kuingia nchini, watatakiwa kutoa taarifa za fedha taslimu wanazosafirisha ikiwa fedha hizo zinalingana au zinazidi kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi (USD 10,000).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni hizo, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema utekelezaji wa kanuni hizi, pamoja na mambo mengine utaiwezesha nchi kuwa na takwimu za usafirishaji fedha taslimu.

“Takwimu hizo zitakazosaidia pamoja na mambo mengine kubaini vitendo vya kihalifu, kupunguza utoroshaji wa mitaji na kuhakikisha kuwa tunapunguza kama siyo kumaliza kabisa usafirishaji wa fedha zitokanazo na uhalifu au/na fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi” alisema Bw. Makombe

Aidha kanuni hizo zimeweka adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakabainika kutaka kupita na fedha zinazolingana au zinazozidi kiwango kilichowekwa bila kutoa taarifa au watakaotoa taarifa za uongo. Alizitaja adhabu hizo kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa fedha taslimu walizonazo na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kama vile kufunguliwa mashtaka.

“Wahalifu pamoja na mambo mengine, wanapenda kusafiri na fedha taslimu kwani wanaogopa kutumia benki kutuma fedha kutokana na umakini unaoongezeka katika benki na udhaifu unaoweza kuwepo mipakani” Alisisitiza Bw. Makombe.Kamishna huyo amewaasa washiriki wa warsha hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kuziba mianya yote ambayo wahalifu wanaweza kuitumia kutimiza kusudi lao ovu na kuhatarisha usalama wa nchi.

Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).





Hivyo makala SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI

yaani makala yote SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/serikali-kudhibiti-usafirishaji-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI"

Post a Comment