WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA
kiungo : WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

soma pia


WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba apeleke wataalamu kwenye kituo cha utafiti kilichopo Makutupora, Dodoma ili wazalishe mbegu bora za ufuta kwa ajili ya mikoa ya kanda ya kati.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya. Waziri Mkuu leo ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

Alikuwa akijibu ombi la mbunge wa viti maalum, Bi. Mariam Ditopile ambaye alisema mkoa wa Dodoma ni wa pili kwa uzalishaji wa ufuta hapa nchini lakini aina ya ufuta inayozalishwa ni ya daraja la chini kwa sababu hawana mbegu za ufuta mweupe.

“Ili mradi mikoa ya kanda ya kati inazalisha ufuta, ninamuagiza Waziri wa Kilimo ahamishe watumishi kutoka kokote ili wakae Makutupora na kuwasaidia wakulima wawe na mbegu bora zenye kutoa mafuta mengi,” alisema.

Amesema kila mwaka Serikali inatumia zaidi ya dola za Marekani milioni 267 kuagiza mafuta ya kula kutoa nje ya nchi na kwamba hivi sasa imeamua kufufua mazao ya mbegu za mafuta ili mafuta ya kula yazalishwe kwa wingi hapa nchini.

 “Sasa hivi tumeanza kufufua mazao ya mbegu za mafuta ni nilianza mkoa wa Kigoma kwa kuhimiza kilimo cha michikichi. Sasa hivi niko Dodoma nahimiza ufuta na alizeti na nitaenda Singida kwa ajili ya zao hilo la alizeti,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.  
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mauno Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chumba cha kuhifadhia maiti, wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Mauno Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk. Ikaji Rashid.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-mkuu-aagiza-watafiti-wa-zao-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA"

Post a Comment