title : RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA
kiungo : RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA
RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC).
Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.
"Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema" alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA
yaani makala yote RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/rais-magufuli-atoa-neno-kwa-mshindi.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI ATOA NENO KWA MSHINDI URAIS KENYA"
Post a Comment