title : WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.
kiungo : WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.
WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.
na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi hiyo hadi tarehe 31 Agosti mwaka huu ili kurahisisha mawasilino kwa wananchi wanao tumia daraja hilo.
Waziri Mhagama ameyasema hayo hapo jana tarehe 19 Julai 2018, alipotembelea katika daraja la Nyerere ili kukagua ujenzi wa barabara hiyo na uendeshaji wa shughuli katika daraja la Nyerere ambapo amesema serikali kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero kwa wananchi wanaovuka kwa miguu na wanaovuka kwa kutumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.(PAUSE-INSERT)
Kwa upande wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio na Mkandarasi wa barabara hiyo, Mhandisi Jamal Mruma wote kwa pamoja wamemuhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa katika daraja na kuweza kuongeza makusanyo ya mapatokatika daraja hilo.
Mbali na gaizo hilo la kukamilishwa kwa barabara , pia
Waziri Mhagama amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuhakikisha unawekwa mfumo bora wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani hapo ili kujua gharama halisi ya tozo ya vyombo vinavyovuka na kuepuka upotevu wa mapato kutokana na kutokuwa
na mfumo wenye kutambua tozo halisi kwa vyombo hivyo.
Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi mwezi Mei mwaka 2016
hadi mwezi Juni 2018, mpaka sasa limeingiza mapato ya takiribani shilingili bilioni 17.1 mapato hayo yanayotokana na tozo kwa vyombo vya usafiri vinavyopita katika daraja hilo.
Imetolewa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF
Angella Msangi.
Hivyo makala WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.
yaani makala yote WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mhagama-ampa-mwezi-mmoja.html
0 Response to "WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE."
Post a Comment