title : FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants)
kiungo : FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants)
FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants)
WATU wengi wamekuwa wakikuta na kuvipita vifaa mithili ya mabomba ya kutoa maji pembezoni mwa barabara, maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, viwanja vya ndege au viwanja vya michezo bila kufahamu vinafanya kazi gani.
Wengine hudhani ni mapambo ya barabara au alama Fulani kwenye maeneo hayo, ambapo baadhi yao hudiriki kuyatumia kinyume na kazi yake kutokana na kutotambua matumizi yake.
Mabomba haya (fire hydrants) sio mapambo bali ni mfumo uliounganishwa na mabomba makubwa ya maji, na kuwa visima vya maji ambapo gari la Zimamoto huchukua maji. Visima hivi vimejengwa makusudi kwa ajili ya kulirahisishia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.
Mabomba hayo (Fire Hydrant) yana msukumo mkubwa wa maji na kusababisha maji yatoke kwa wingi na kwamuda mfupi. Uwepo wa vifaa hivyo sehemu mbalimbali za makazi ya watu na maeneo mengineyo hurahisisha zoezi zima la uzimaji moto, kwani pindi gari la kuzima moto linapoishiwa maji hujazwa hapohapo badala ya kuyafuata mbali na eneo la tukio.
Hivyo makala FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants)
yaani makala yote FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/fahamu-visima-vya-uzimaji-moto-fire.html
0 Response to "FAHAMU VISIMA VYA UZIMAJI MOTO (fire hydrants)"
Post a Comment