title : TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B
kiungo : TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B
TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B
Zoezi la upimaji likiendelea ili kuweza kuonyesha mawe ya upimaji kabla ya kumkabidhi Mwananchi husika mapema leo katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola.
Mmoja wa Wananchi kutoka Kipunguni ambaye ameoneshwa eneo lake akiwa amepiga picha katika eneo hilo Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Baadhi ya Wananchi wa Kipunguni Mashariki na Kipunguni A wakiwa na Maofisa wakisubiri kupimiwa maeneo yao katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Picha na.
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Ilala,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Kampuni ya Tanzania Remix imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye juu ya ulipaji wa fidia ya Viwanja kwa Wananchi wa Kata ya kipunguni A na Kipunguni mashariki.
Agizo hilo alilotoa Agosti 30 mwaka huu limeanza kutekelezwa leo kwa Wananchi watokao Kipunguni Mashariki na Kipunguni A kwenda mtaa wa Kidole na Luhanga kupewa viwanja 537 ndani ya kata ya Msongola ili kupisha mradi wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA).
Awali Mhandisi Nditiye alitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw, Richard Mayongela kushirikiana na Manispaa ya Ilala ,Mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Tanzania Remix ambayo ilihusika na upimaji wa maeneo hayo kuhakikisha inawagawia Wananchi viwanja hivyo na kuhakikisha viwanja hivyo vina ubora.
“Mshirikiane na Tanzania Remix na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa kuwagawia Wananchi viwanja hivi vilevile shirikianeni na vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini wafanyakazi wote wa TAA waliojiingiza kwenye mradi huu na kujipatia viwanja kinyume na utaratibu angali hawakuguswa na mradi huu wabainishwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria”alisema.
Safari Kishiwa na Evaline Malume ni miongoni mwa Wananchi walioanza kugawiwa viwanja hivyo nakuishukuru Serikali kutokana na maeneo hayo kuwa katika mazingira mazuri.
Wananchi hao walidai wanawashangaa baadhi ya wananchi wenzao walioathiriwa na mradi huo kukimbilia mahakamani kwasababu mbalimbali zisizo na mashiko.
"Tuwaombe tu wenzetu wafute kesi waje wachukue viwanja viwanja hivi vipo kwenye mazingira mazuri tofauti na wanavyofikiri"walisema.
Hivyo makala TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B
yaani makala yote TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/taa-manispaa-ya-ilala-tanzania-remix.html
0 Response to "TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA KWA WANANCHI WA KIPUNGUNI B"
Post a Comment