title : WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE
kiungo : WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE
WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE
Na Agness Francis wa Globu ya Jamii
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amewatia mbaroni wahalifu wa makundi ya ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Vibaka hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa umri wao ni kati ya miaka 12-25, opresheni hiyo ilikamata wahalifu 8 kutoka Mbande na wengine 8 kutoka Chamazi wilayani humo.
Hata hivyo wahalifu hao walikiri kuwa makundi na vishawishi ndio huwasababishia kufanya matukio hayo kwa kutumia visu na mapanga kwa kupora pochi za kina mama kuchukua simu pamoja na fedha.Vile vile alikemea utoro wa wanafunzi na kutaka wazazi kurejeshe watoto mashuleni na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi katika kupata elimu.
Nae mzazi Zuhura Hamza alizungumza` kwa kusema watoto wenyewe ndio hawasikii hawataki kusoma wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini hawajapata suluhu la tatizo hilo hivyo akiomba msaada kwa wakuu wa shule.
Kamanda Muruto alitoa wito kwa wazazi wawahimize watoto kwenda shule, kwani watoto wamezagaa mitaani na kujiingiza katika makundi mabovu kama ya madawa ya kuevya, uporaji, uvuataji bangi na sigara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwashikilia watuhumiwa wa makundi ya ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja na wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akiwaonesha wanahabari watuhumiwa wa makosa mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Hivyo makala WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE
yaani makala yote WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/watuhumiwa-wa-makosambalimbali-mbaroni.html
0 Response to "WATUHUMIWA WA MAKOSAMBALIMBALI MBARONI TEMEKE"
Post a Comment