Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka

Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka
kiungo : Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka

soma pia


Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka

Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashimu Mgandilwa azindua mpango Kabambe wa uchangiaji uzoaji taka kwa kwenye wilaya hiyo, ambapo kila kaya itatakiwa kutoa shilingi mia moja kwa siku sawa na 3000 kwa mwezi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam DC Mgandilwa ameeleza kuwa mpango huo utasaidia kupunguza suala la uchafu katika wilaya hiyo na gharama zake ni nafuu tofauti na awali ambapo kaya moja kwa kata ya Kibada walilazimika kulipa kiasi cha shilingi elfu 20000 mpaka 40000 jambo ambalo ni changamoto kwa wakazi hao.
 DC Mgandilwa ameeleza kuwa mradi huo utasaidia changamoto iliyojitokeza ya baadhi ya watu kutupa taka kwenye fukwe ya bahari, huku akiwaomba wananchi katika kaya mbalimbali kutunza taka zinazozalishwa majumbani mpaka magari ya mradi yatakapokuja kuzichukua zikiwa katika mazingira mazuri, ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutaifanya wilaya ya Kigamboni kuepuka Magonjwa ya mlipuko.
DC Mgandilwa ameisisitiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha mradi huo unakuwa ni wa uhakika kwa kutosuasua na kuhakikisha kata zinazolewa kwa wakati na hayo magari manne ya awali yasambazwe maeneo mbalimbali ili huduma stahiki ziwafikie wananchi.


 DC Mgandilwa ameongeza kuwa Halmashauri haina uwezo wa kutoa msisitizo kila wakati ili watu watunze Mazingira  hivyo ni jukumu la wanakigamboni kutunza mazingira, ambapo amewaomba  wananchi kulipa kiasi hicho cha 3000 kwa mwezi kiasi ambacho mwananchi wa kawaida anaweza kumudu, vile vile kwa wamiliki wa Hoteli na taasisi mbalimbali wamewekewa kiasi ambacho ni nafuu kwao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Steven Katemba ameeleza kuwa mradi huo utawanufaisha vijana zaidi ya 134 na utaanza kwa kata tano ikiwemo Kigamboni, Mjimwema, Tungi, Kibada na Vijibweni.
Huku akieleza kuwa mpango wa baadae ni kuwa na Dampo la Lingato  ambapo bilioni moja imetengwa na Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya ukarabati wa dampo hivyo ndani ya miezi kadhaa ukarabati utakwisha na taka hazitakuwa zinapelekwa Kata ya Tungi.


Hivyo makala Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka

yaani makala yote Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/wakazi-wa-kigamboni-kuchangia-shilingi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wakazi wa Kigamboni kuchangia shilingi 100 ada ya usafi ya uzoaji taka"

Post a Comment