title : MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA
kiungo : MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA
MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.
Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.
“Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.
“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.
Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.
“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilizia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS
Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA
yaani makala yote MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/maonesho-ya-sabasaba-2017-waziri-wa.html
0 Response to "MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA"
Post a Comment