SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA

SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA
kiungo : SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA

soma pia


SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA

SHINDANO la ngoma za utamaduni liitwalo ‘Mavunde na utamaduni wetu’ limefanyika leo mjini Dodoma likiwa na lengo la kuenzi, kulinda na kuhifadhi utamaduni wa watu wa Dodoma.

Shindano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na lilihusisha vikundi vya ngoma za asili ya Dodoma 7.Vikundi hivyo ni Simba dume, changamoto, Noti mtemi, Neema Yerusalem, Chipukizi, Finga Vikonje na Imani Makulu.

Akizungumza katika shindano hilo, Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema uwepo wa shindano hilo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2015 na kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuhamishia shughuli za serikali Dodoma, kupiga vita Rushwa na Ubadhirifu na Kulinda Maliasili za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.

“Tamaduni zetu zilikuwa zimeanza kusahaulika watu hawakuona tena umuhimu wa ngoma za jadi na hii ni kutokana na utandawazi na kuwa watu wa mjini sana tumesahau tumetoka wapi,”amesema Mavunde.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu lililofanyika mjini Dodoma.
Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu, mjini Dodoma 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akiwa na viongozi mbalimbali katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu. 
Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoshiriki katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.



Hivyo makala SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA

yaani makala yote SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/shindano-la-mavunde-na-utamaduni-wetu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA"

Post a Comment