title : OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI
kiungo : OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI
OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kitengo cha ardhi , imemtaka Msajiri wa Hati wa Wizara ya Ardhu,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuta mara moja hati namba 105525 wa Kiwanja namba 1003 kilichopo Mtaa wa Sekenke Kinondoni, chenye mgogoro uliodumu kwa miaka 10.
Kiwanja hicho kilikuwa kinagombewa na wananchi wawili ambao ni Ally Abdi na Seleman Marashed kutokana na familia kukiuza mara mbili huku pia kikiwa na namba mbili ambazo ni 212 na 1003.Ofisi hiyo imebaini kunaupindishaji mkubwa wa taratibu za uuzwaji na upimaji wa kiwanja hicho ambacho kilikuwa ni mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya mkuu wa mkoa kwenda Wizara ya Ardhi, iliyosainiwa na Ofisa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Edgar Msolla, ya Februari 15 mwaka huu, baada ya uchunguzi mzito kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni ilibaini kuwepo ukiukwaji wa sheria.Uchunguzi huo umekuja baada ya Abdi kuwasilisha malalamiko katika ofisi hiyo kuhusu kiwanja hicho namba 212 ambacho kipo kwenye mchoro wenye Survey Plan D1.503/23 wa mwaka 1994.
Kiwanja hicho kina ofa iliyotolewa Aprili 18 mwaka 1964 kwa NHC ambao walikiuza kwa Moshi Majungu akiwa msimamizi wa mirathi ya baba yake Kondo Majenga.Abdi anadaiwa kununua kiwanja hicho mwaka 2004 kutoka kwa Moshi Kondo Majenga kwa niaba ya familia ya Kondo Majengo.Hata hivyo baada ya taratribu za mauziano hayo taratibu za kuhamisha miliki hazikukamilika.Imedaiwa kwa mara ya pili kiwanja hicho kiluzwa kwa tena na Moshi Mussa Majenga aliyeuwa msimamizi wa mirathi ya Kondo Majenga kwa Marshed mwaka 2008.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kinondoni Mjini,Mussa Embe akizungumza na waandishi wa habari nakufafanua kwamba mtaa wake unanyumba unanamba za nyumba nyumba 490 tu.
Ally Abdi akinonesha nyaraka mbalimbali za nyumba hiyo aliyo.
Hivyo makala OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI
yaani makala yote OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/ofisi-ya-mkuu-wa-mkoa-dar-yaiagiza.html
0 Response to "OFISI YA MKUU WA MKOA DAR YAIAGIZA WIZARA YA ARIDHI KUFUTA HATI KIWANJA NAMBA 105525 KILICHOPO KINONDONI"
Post a Comment