title : RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
kiungo : RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma
RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.

Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa.
"Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote"alisema Magufuli.Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za Wananchi zilizo kuwa zikiibiwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao.
"Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua wewe sio tumbili ,matumbili ni wao wewe najua ni wa Chama kingine lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwahiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza kitu ulichokifanya ni kikubwa Kwa,Taifa naomba nikupongeze kwa hilo",
Alisema Kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi , hivyo atahakikisha kuwa Wananchi hawateseki na Wale ambao wameiba fedha za serikali na Wananchi wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo, ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo.
Hivyo makala RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
yaani makala yote RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-amfagilia-kafulila.html
0 Response to "RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO"
Post a Comment