NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba

NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba
kiungo : NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba

soma pia


NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba

Watoto wakifurahi baada ya wazazi wao kuwasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Na Grace Michael

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekuwa mshindi wa tatu kupitia kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ushindi uliotangazwa mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 41 ya Sabasaba.

NHIF inayoendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya umri wa miaka 18 kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwa ajili ya kuwahakikishia watoto hao upatikanaji wa huduma za matibabu wakati wote.

Hata hivyo mpango wa Toto Afya Kadi umekuwa kivutio kikubwa katika Maonesho hayo ambapo wananchi wengi wanamiminika bandani hapo kwa lengo la kupata huduma kwa ajili ya watoto wao.

Wakizungumza bandani hapo wananchi, wamesema kampeni hii ni mkombozi mkubwa kwa familia ambazo zina watoto na hazikuwa na fursa ya kujiunga na huduma za NHIF hapo awali.

Wamesema utaratibu huu uendelee katika maeneo mengi zaidi ili watoto wote wa Tanzania wawe ndani ya Mfumo wa kupata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya.

Akizungumzia hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Anjela Mziray, amesema kuwa NHIF imejipanga kuhakikisha inafika kila mahali kwa lengo la kuwahudumia Watanzania wote.

“NHIF tumejipanga na tunakwenda sambasamba na kasi ambayo Mkuu wetu wan chi Rais Dk. John Pombe Magufuli anaitaka hususan katika kuwahakikishia wananchi huduma za matibabu hivyo Watanzania wote tutawafikia katika maeneo yao,” alisema.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya una mtandao mpana wa vituo vya kutoa matibabu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wanachama wake.
Watoto wakifurahi baada ya wazazi wao kuwasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mmoja wa Wazazi akiwa na watoto wake ambao amewasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi. Bofya hapa kuona picha zaidi 


Hivyo makala NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba

yaani makala yote NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/nhif-yaibuka-na-ushindi-maonesho-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba"

Post a Comment