title : NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA.
kiungo : NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA.
NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa NHIF akipokea cheti cha ushindi Kutoka kwa Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo wakati wa maonesho ya nanenane Dodoma.
Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja.
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umeibuka kidedea miongoni mwa mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoshiriki maonesho ya kumi ya kilimo na ufugaji inayoendelea Mkoani Dodoma.
Katika maonesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya kanda ya kati ya Dodoma na Singida mfuko wa NHIF ulishika nafasi ya tatu kwa utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.
Akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi mbalimbali waliofanya vizuri katika maonesho hayo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI), Mh.Selemani Jafo amepongeza jitihada za NHIF na mifuko mingine katika juhudi zao za kumkomboa mtanzania katika nyanja mbalimbali.
“Lengo letu ni kuyafanya maonesho haya ya nane nane hapa Dodoma yawe ya kimataifa, hivyo tunatambua mchango wa washiriki wote katika kumsaidia mkulima na mfugaji,” amesema Mh.Jafo
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF Anjela Mziray amesema tuzo hiyo ni kichocheo kwa mfuko huo katika kuboresha maisha ya Mtanzania.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti maalumu kutoka kwa Mh.Jafo,Bi Anjela Mziray ameshukuru kamati ya maandalizi ya maonesho hayo kutambua mchango wa mfuko wa NHIF.
“Tuzo hii kwetu ni motisha tosha ,na pia itatukumbusha kuwa tuna deni la kuwahudumia Watanznia tulichokionesha kwenye maonesho hayo ndio majukumu yetu ya kila siku,” amesisitiza Bi.Mziray.
Pamoja na hilo Bi Mziray amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kutembelea Ofisi ya NHIF mkoani humo iliyopo jengo la Hazina Ndogo, barabara ya UDOM ili kujipatia huduma zinazotolewa na mfuko huo.
Maonesho ya Nane Nane kanda ya kati yamehairishwa leo lakini kutokana na maombi ya wadau Mh.Jafo ameongeza siku mbili zaidi ili kutoa fursa zaid kwa wananchi wa kanda ya kati na maeneo jirani kuendelea kupata huduma.
Hivyo makala NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA.
yaani makala yote NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/nhif-umeibuka-kidedea-miongoni-mwa.html
0 Response to "NHIF UMEIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII ILIYOSHIRIKI MAONESHO YA KUMI YANANENANE MKOANI DODOMA."
Post a Comment