MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA
kiungo : MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

soma pia


MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

Mshabiki wa Sunderland Bradley Lowery (6) amezikwa leo na mamia ya mashabiki wa timu hiyo pamoja na wachezaji wa Sunderland wakionyesha masikitiko makubwa kwa kuondokewa na moja ya mashabiki wao wakubwa.Bradley alifariki Ijumaa wiki iliyopita baada ya kuugua saratani kwa muda.ambapo katika uhai wake alikuwa mshabiki mkubwa wa timu ya Sunderland na ilifikia kipindi baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Jermain Defoe kwenda kumjulia hali katika hopsitali aliyokuwa amelazwa.Mchezaji Jermain Defoe, ambaye aliunda urafiki wa karibu sana na Bradley, aliungana na familia ya mvulana huyo kumuaga kwa mara ya mwisho.
Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa la Mtakatifu Yusufu kijijini mwao, wengi wakimsifu sana mvulana huyo kwa ukakamavu wake na sifa alizojilimbikizia.Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana. Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na haingeweza kutibiwa.
Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.
Habari kwa hisani ya BBC Swahili.

Aliyekuwa Kocha wa Sunderland David Moyes katika msiba wa Bradley Lowery.
Ujumbe wa Bradley ukiwa umewekwa katika moja ya barabara


Hivyo makala MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA

yaani makala yote MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/mashabiki-wa-sunderland-bradley-lowery.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MASHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY AZIKWA NA MAMIA YA WAINGEREZA"

Post a Comment